Nyumbani Home
Utapata ukumbusho wa ada, vikao na matangazo moja kwa moja kwenye simu. You will get reminders about dues, meetings and notices straight to your phone.
Salio langu My statement
Deni = MADAI − MALIPO. Hakuna salio linalohifadhiwa popote; kila namba hapa inahesabiwa upya kutoka kwenye kumbukumbu. Debt = CHARGES − PAYMENTS. No balance is stored anywhere; every figure here is worked out again from the ledger.
Lipa moja kwa moja kwenye akaunti ya CRDB 0133608480600, kisha jaza hapa ili Katibu athibitishe. Deni lako litapungua mara moja. Pay directly into the CRDB account 0133608480600, then fill this in so Katibu can verify it. Your debt drops right away.
Matangazo Notices
Vikao Meetings
Wasifu wangu My profileAkaunti yangu My account
Kila mara faili lako linapofunguliwa na mtu mwingine, inaandikwa hapa —
nani, lini, na kwa sababu gani.
Every time somebody else opens one of your files it is recorded here:
who, when, and on what authority.
Unaweza kumruhusu kiongozi aone nyaraka zako, na kuondoa ruhusa wakati wowote. You may let an officer see your documents, and withdraw that permission at any time.
Katiba ConstitutionAkaunti yangu My account
TUMAINI GROUP
KATIBA
Hati rasmi ya umoja — maandiko asilia kwa Kiswahili. The group's official document — original text in Swahili.
UTANGULIZI
TUMAINI GROUP ni umoja ulionzishwa na wana ndugu kutoka mkoa wa Kagera waishio Dar es Salaam. Hivyo waliamua kuunda umoja wenye uwezo na nguvu ambao utapanga mikakati na kusimamia maendeleo yao chini ya katiba imara.
KANUNI
- Mkutano mkuu au mkutano wa wanaumoja utatayarisha kanuni ambazo zitasaidia kuangalia na kurahisisha utekelezaji wa masharti na wajibu katika katiba hii.
- Kanuni zitakazotungwa hazitapingana na katiba na endapo itatokea basi katiba ndiyo itakayotoa mwanga sahihi.
- Baada ya mwombaji kuandika barua na kukubaliwa pamoja na kulipa michango yake kwa mujibu wa katiba atalazimika kujaza fomu binafsi; pia mwombaji kabla ya kukubaliwa itambidi awe na mdhamini ndani ya umoja ambaye ni mwana umoja.
- Kila mwisho wa mwezi wa sita na mwisho wa mwaka mtunza fedha wa umoja atasoma taarifa ya mapato na matumizi ya umoja; hivyo kabla ya kuwasilisha hiyo taarifa kwa wanaumoja itabidi wateuliwe wajumbe wawili wenye taaluma ya hesabu ili waweze kukagua na kuthibitisha hizo hesabu ambazo ataziwasilisha mtunza fedha.
MADHUMUNI YA UMOJA
- Kuinua na kuimarisha nguvu za kiuchumi za wanaumoja.
- Kujenga na kuimarisha ushirikiano katika nyanja mbali mbali za kiuchumi na kijamii.
- Kusaidiana baina ya wanaumoja katika shida na raha.
- Kuanzisha miradi mbali mbali ya kiuchumi na kijamii kwa manufaa ya wanaumoja na jamii ya Watanzania kwa ujumla.
MWANA UMOJA
Mwana umoja anaweza kuwa mwana Kagera yeyote mwenye umri wa miaka 18 na kuendelea, mwenye akili timamu, anayekubaliana na madhumuni ama malengo ya umoja, ambaye atakuwa amefuata taratibu za kujiunga na umoja huu.
KUOMBA UANAUMOJA
Mwana Kagera yeyote anaweza kuomba uanaumoja kwa kuandika barua ya maombi itakayojadiliwa na kamati tendaji kwa kukubali au kukataa.
HAKI NA WAJIBU WA MWANAUMOJA
- Kuchagua au kuchaguliwa katika ngazi zote za uongozi wa umoja.
- Kuhudhuria na kushiriki katika mikutano yote ya umoja na shughuli zote za umoja.
- Kuhudumiwa na umoja katika mambo anayostahili kuhudumiwa kwa mujibu wa katiba hii na kanuni zake.
KIKOMO CHA WANAUMOJA
Uanaumoja utakoma endapo:—
- Mwanaumoja akifariki.
- Mwanaumoja akijiondoa kwa hiari yake.
- Mwanaumoja akishindwa kulipa ada katika kipindi cha miezi mitatu mfululizo.
- Mwanaumoja akishindwa kuhudhuria vikao vitatu mfululizo bila taarifa ya msingi.
- Mwanaumoja akitenda kosa la jinai wakati wa mikutano au mikusanyiko ya umoja.
- Mwanaumoja akiwa na malimbikizo ya michango yote kwa kiwango kinacholingana na miezi mitatu.
- Mwanaumoja akihama nje ya Dar es Salaam.
VIONGOZI
- Umoja utakuwa na viongozi wafuatao:—
- Mwenyekiti
- Makamu mwenyekiti
- Katibu
- Katibu msaidizi
- Mweka hazina
- Viongozi wote watachaguliwa na mkutano mkuu wa umoja na watakaa madarakani kwa kipindi cha miaka 2. Uchaguzi utakuwa unafanyika mwezi January.
- Kutakuwa na kamati ya utendaji ambapo wajumbe wake watakuwa ni wale waliotajwa katika 9(a) pamoja na wajumbe watatu wa kuchaguliwa.
MKUTANO NA VIKAO VYA UMOJA
- Kutakuwepo na mkutano mkuu ambao ndio utakuwa kikao cha juu katika umoja wenye madaraka ya kufanya kila aina ya maamuzi.
- Kutakuwepo na mkutano wa wanaumoja utakaofanyika mara moja kila baada ya miezi 2, siku ya Jumapili ya 2 ya mwezi.
- Vikao vya kamati ya utendaji vitafanyika mara moja kwa kila mwezi.
- Endapo kutatokea dharura kutakuwepo vikao vya dharura vya wanaumoja au kamati ya utendaji.
KAZI YA MKUTANO NA VIKAO VYA UMOJA
- Mkutano mkuu
- Ndicho chombo cha juu katika maamuzi ya umoja.
- Kufanya na kupitisha marekebisho ya katiba na kanuni.
- Kuchagua viongozi.
- Kusimamia fedha na matumizi yake.
- Mkutano wa wanaumoja
- Kupokea, kujadili na kupitisha mapendekezo ya kamati ya utendaji.
- Kurekebisha au kubadili kanuni.
- Kumkubali au kumfukuza mwanaumoja.
KAMATI YA WADHAMINI
Mkutano wa wanaumoja utawachagua wadhamini wa mfuko wa umoja wasiopungua watatu na wasiozidi watano.
AKIDI — (IDADI)
Akidi itakuwa ni moja ya nne (1/4) ya wanaumoja.
ADA NA MICHANGO
Kila mwanaumoja atawajibika kulipa kiingilio, ada na michango yote kadri ya kanuni na katiba hii.
AKAUNTI YA BENKI
Umoja utakuwa na akaunti ya benki itakayopendekezwa na mkutano wa wanaumoja.
MABADILIKO YA KATIBA
Katiba hii itarekebishwa, kubadilishwa, kuondolewa au kuongezwa kifungu chochote na mkutano mkuu.
MWISHO WA UMOJA
Umoja unaweza kuvunjwa baada ya azimio la kufanya hivyo kupitishwa na wanaumoja hai kwa idadi 3/4.
Kanuni RegulationsAkaunti yangu My account
TUMAINI GROUP
KIAMBATANISHO — (KANUNI)
Umoja utakuwa na kanuni zifuatazo. Maandiko asilia kwa Kiswahili. The group's regulations. Original text in Swahili.
MWANAUMOJA MPYA
Mwanaumoja mpya atathibitishwa baada ya miezi sita (6) na kabla ya hapo hatahudumiwa na umoja, isipokuwa ataruhusiwa kuhudhuria vikao/mikutano, sherehe, kupiga kura na shughuli yoyote ya umoja. Pia mwanaumoja mgeni katika kipindi cha uangalizi atalazimika kulipa ada ya kila mwezi na michango mingine ya umoja kulingana na katiba.
KUSAIDIWA WAKATI WA MAAFA NA RAHA
- Wanaohusika kusaidiwa wakati wa kifo ni:—
- Mwanaumoja
- Mtoto wa mwanaumoja
- Baba / Mama wa mwanaumoja
- Mume / Mke wa mwanaumoja
- Baba mkwe / Mama mkwe wa mwanaumoja
- Mtu mmoja tegemezi wa mwanaumoja
- Wakati wa maafa, kifo na raha michango itakuwa kama ifuatavyo:—
- Endapo waliotajwa katika 2(a)(i)–(vi) watafariki, umoja utatoa kiasi cha pesa kulingana na kiwango kitakachokuwa kimekubaliwa kwa wakati huo kumpa mhusika.
- Endapo waliotajwa 2(a)(i)–(vi) wataugua na kulazwa hospitali kwa muda zaidi ya siku tatu, umoja utatoa kiasi cha Tsh 200,000/= (laki mbili) kumpa mhusika.
- Waliotajwa 2(a)(i)–(vi) endapo wataoa au kuolewa, mhusika itabidi atoe taarifa kwenye umoja kabla ya miezi mitatu shughuli hiyo kufanyika; hivyo kila mwana umoja atalazimika kushiriki katika maandalizi ya harusi (kamati) kwa kuchangia kiasi kitakachokubalika na kamati ya sherehe hiyo. Pia umoja utatoa kwenye mfuko wa umoja kiasi cha pesa kitakachokubalika kununua zawadi ya mhusika.
- Endapo mwanaumoja atajifungua mtoto, umoja utampa Tsh 200,000/=.
ADA NA MICHANGO
- Mwana umoja mpya atalipa kiingilio Tsh 200,000/= na hicho kiingilio kilipwe ndani ya miezi mitatu.
- Ada itakuwa Tsh 20,000/= kwa kila mwezi.
ADHABU NA FAINI
Mwanaumoja atatozwa faini zifuatazo:—
- Kuchelewa zaidi ya nusu saa (dakika 30) kwenye vikao — Tsh 500/=.
- Kuvuruga vikao — Tsh 1,000/=.
- Kutohudhuria vikao bila kutoa udhuru unaoambatana na uthibitisho — Tsh 5,000/=.
- Kutoa taarifa za uongo — Tsh 5,000/=.
- Kutoshiriki katika matatizo bila taarifa — Tsh 5,000/=.
KUITISHA VIKAO
Vikao vyote vitaitishwa na mwenyekiti baada ya kushauriana na katibu.
MADARAKA NA WAJIBU WA VIONGOZI
- Mwenyekiti
- Atakuwa msemaji mkuu wa umoja.
- Atakuwa msimamizi mkuu wa shughuli za umoja.
- Ataitisha vikao.
- Ataandaa na kusoma taarifa ya mwaka.
- Atakuwa na kura ya turufu.
- Mwenyekiti msaidizi — atafanya kazi zote za Mwenyekiti kama hatakuwepo au atakavyoagizwa na M/Kiti.
- Katibu
- Atakuwa mtendaji mkuu wa umoja.
- Atatunza kumbukumbu za umoja.
- Ataandaa agenda na mikutano kwa kushirikiana na Mwenyekiti.
- Katibu msaidizi — atafanya kazi zote za katibu endapo hatakuwepo au atakavyoagizwa na katibu.
- Mweka hazina
- Atatunza na kuweka kumbukumbu zote za fedha.
- Atadai madeni yote ya umoja.
- Atatoa taarifa ya fedha kila baada ya miezi miwili.
MAKATO YA MADENI
Madeni anayodaiwa mwanaumoja yatakatwa kwanza kabla ya kupewa huduma.
MADENI YA MWISHO WA MWAKA
Kila mwanaumoja atalazimika kulipa madeni yake yote kila mwisho wa mwaka.
MAJANGA (MOTO / MAFURIKO YA MAJI)
Ikitokea mwana umoja amepatwa na janga mojawapo kati ya hayo yaliyotajwa hapo juu, umoja utalazimika kumpa msaada wa pesa muhanga huyo kwa namna umoja utakavyoona ukubwa wa janga hilo.
SHEREHE YA UMOJA
Kutakuwa na sherehe ya umoja ya kufunga mwaka ambayo itafanyika kila mwisho wa mwaka; hivyo umoja utakaa na kupendekeza siku ya kufanya sherehe.
Sera ya Faragha Privacy policyAkaunti yangu My account
TUMAINI GROUP
SERA YA FARAGHA
Taarifa zako ni za nini, nani anaziona, na kwa mujibu wa kifungu gani. What your data is for, who can see it, and under which article.
Mfumo huu ni nini — What this system is
Hii ni app ya kumbukumbu na mawasiliano ya TUMAINI GROUP: salio na michango, matangazo, vikao, wasifu na nyaraka za utambulisho. Inaendeshwa na viongozi wa umoja kwa madaraka waliyopewa na , kwa madhumuni ya umoja yaliyoainishwa katika . This is TUMAINI GROUP's record-keeping and communication app: balances and contributions, notices, meetings, profiles and identity documents. It is run by the group's officers under the powers in , for the purposes set out in .
Taarifa tunazotunza — What we keep
- Jina, mawasiliano na taarifa za wasifu unazojaza mwenyewe — zinahitajika kwa uanachama kwa mujibu wa (fomu binafsi na mdhamini). Name, contacts and the profile details you fill in yourself — required for membership under (personal form and a guarantor).
- Namba ya NIDA na nakala za vitambulisho unavyopakia (picha au PDF) — kwa uthibitisho wa mwanachama kama inavyotaka. Your NIDA number and the identity documents you upload (photo or PDF) — to verify membership as requires.
- Kumbukumbu za malipo: kiingilio, ada za mwezi, michango na faini — kwa mujibu wa , na . Payment records: entry fee, monthly dues, contributions and fines — under , and .
- Vikao vilivyopangwa na matangazo yaliyotumwa, pamoja na nani aliyetuma au kuhariri nini. Meetings scheduled and notices sent, including who sent or edited what.
- Taarifa za kuingia: namba ya simu na PIN yako (imefichwa kwa "hash" — hakuna anayeweza kuisoma), pamoja na usajili wa arifa za simu (push) ukiziruhusu. Sign-in data: your phone number and PIN (stored hashed — nobody can read it back), plus your push-notification subscription if you allow alerts.
- Kumbukumbu za nani-alifungua-nini: kila nyaraka yako ya utambulisho ikifunguliwa na kiongozi, tukio hilo linarekodiwa. Who-opened-what records: every time an officer opens one of your identity documents, that event is logged.
Nani anaona nini — Who sees what
- Wewe unaona salio lako, wasifu wako, nyaraka zako, na orodha ya waliofungua nyaraka zako. You see your own balance, profile, documents, and the list of who has opened your documents.
- Viongozi wanaona kile tu wajibu wao unahitaji, kwa mgawanyo wa : Mweka hazina — kumbukumbu za fedha; Katibu — kumbukumbu za umoja; Mwenyekiti — usimamizi. Officers see only what their duty requires, per the division in : the Treasurer — financial records; the Secretary — the group's records; the Chair — oversight.
- Nyaraka za utambulisho hufunguliwa kwa IDHINI YAKO — wewe ndiye unayemruhusu kiongozi, kwa muda unaouchagua. Dharura ya kweli pekee ndiyo huruhusu ufunguzi bila idhini, nao unarekodiwa na kuonekana kwako wazi. Identity documents open with YOUR CONSENT — you grant an officer access, for a period you choose. Only a genuine emergency allows an opening without consent, and that opening is logged and visibly shown to you.
- Hakuna taarifa inayotoka nje ya umoja: hatuuzi data, hakuna matangazo ya kibiashara, hakuna kampuni ya tatu inayopewa taarifa zako. Nothing leaves the group: we do not sell data, there is no advertising, no third-party company receives your information.
Zinatunzwa vipi — How it is protected
Taarifa zote husafiri kwa njia iliyofungwa (HTTPS) na kutunzwa kwenye seva ya umoja. PIN huhifadhiwa kwa hash isiyorudishika. Kila hatua ya kiuongozi — kutoa nafasi, kurekodi malipo, kuthibitisha nyaraka — inaacha kumbukumbu ya ukaguzi yenye jina na tarehe, kwa roho ile ile ya ukaguzi wa hesabu ya . All data travels encrypted (HTTPS) and lives on the group's server. PINs are stored as irreversible hashes. Every officer action — issuing a slot, recording a payment, verifying a document — leaves an audit record with a name and a date, in the same spirit as the accounts inspection of .
Zinakaa muda gani — How long it is kept
Taarifa zako hukaa mfumoni muda wote wa uanachama wako. Uanachama ukikoma kwa mujibu wa , kumbukumbu za fedha hubaki kwenye hesabu za umoja (ni sehemu ya taarifa za mapato na matumizi), na taarifa nyingine za binafsi huacha kutumika. Your data stays for as long as your membership does. When membership ends under , financial records remain part of the group's accounts (they belong to the income and expenditure record), and other personal details fall out of use.
Haki zako — Your rights
- Kuona na kusahihisha wasifu wako wakati wowote, ukurasa wa Wasifu. See and correct your profile at any time, on the Profile page.
- Kuona nani amefungua nyaraka zako, na kuondoa idhini uliyotoa — wakati wowote. See who has opened your documents, and withdraw any consent you have given — at any time.
- Kuuliza au kupinga jambo kupitia Katibu au ukurasa wa Maswali — haki yako ya kuhudumiwa ni ya . Ask or challenge anything through the Secretary or the Questions page — your right to be served is .
Mabadiliko ya sera hii — Changes to this policy
Mfumo unapoongeza kipengele kinachogusa taarifa zako, sera hii husasishwa sambamba nacho na toleo jipya kutangazwa kwenye Matangazo. Msingi hauhami: Katiba ndiyo yenye kauli ya mwisho — — na mabadiliko ya msingi ni ya Mkutano Mkuu kwa . When the system gains a feature that touches your data, this policy is updated alongside it and announced in Notices. The foundation does not move: the Constitution has the final word — — and fundamental changes belong to the General Meeting under .
Masharti ya Matumizi Terms of useAkaunti yangu My account
TUMAINI GROUP
MASHARTI YA MATUMIZI
Kutumia app hii ni kukubali masharti haya — nayo yanasimama juu ya Katiba na Kanuni. Using this app means accepting these terms — and they stand on the Katiba and Kanuni.
Kukubali masharti — Acceptance
App hii ni ya wanachama wa TUMAINI GROUP. Kuitumia ni kukubali masharti haya pamoja na Katiba na Kanuni za umoja kwa ujumla wake. Panapotokea mkanganyiko kati ya mfumo na Katiba, Katiba inashinda — . This app belongs to the members of TUMAINI GROUP. Using it means accepting these terms together with the group's Constitution and Regulations in full. Where the system and the Constitution ever disagree, the Constitution wins — .
Akaunti yako — Your account
- Akaunti hutolewa kwa mwanachama aliyekubaliwa kwa taratibu za na , kupitia nafasi/kadi inayotolewa na viongozi. Mwanachama mpya yuko kwenye kipindi cha uangalizi cha miezi sita kwa . An account is issued to a member admitted under and , through a slot/card issued by the officers. A new member is on the six-month probation of .
- PIN yako ni siri yako: usimpe mtu yeyote, na kila kinachofanywa kupitia akaunti yako kinahesabika kuwa ni chako. Your PIN is yours alone: share it with nobody, and whatever is done through your account counts as done by you.
- Taarifa unazoweka lazima ziwe za kweli — taarifa za uongo zina faini ya . What you enter must be true — false information carries the fine in .
Wajibu wako — Your obligations
- Kulipa kiingilio, ada na michango kwa viwango na muda wa na ; madeni hulipwa yote kila mwisho wa mwaka — . Pay the entry fee, dues and contributions at the rates and times of and ; all debts clear at each year's end — .
- Kuhudhuria vikao vinavyotangazwa humu — kutokuhudhuria bila udhuru kuna faini za , na vikao vitatu mfululizo bila taarifa ni kikomo cha uanachama kwa . Attend the meetings announced here — unexcused absence carries the fines of , and three consecutive absences without notice end membership under .
- Kutumia app kwa heshima: usipakie nyaraka za mtu mwingine, usitume matangazo ya uongo, usijaribu kuingia kwenye akaunti isiyo yako. Use the app honestly: do not upload someone else's documents, send false notices, or attempt to enter an account that is not yours.
Matumizi ya viongozi — Officer use
Viongozi hutumia kurasa za uongozi kwa mipaka ya : vikao huitishwa na Mwenyekiti baada ya kushauriana na Katibu — ; kumbukumbu za fedha huwekwa na Mweka hazina; nafasi za kujiunga hutolewa kwa kikao kilichoidhinisha. Kila hatua inarekodiwa kwa jina la aliyeifanya. Officers use the officer pages within the bounds of : meetings are convened by the Chair after consulting the Secretary — ; financial records are kept by the Treasurer; joining slots are issued against an authorising meeting. Every action is recorded under the name of whoever took it.
Huduma na msaada — Services and benefits
Misaada ya maafa na raha hufuata , na ya majanga . Kabla ya huduma yoyote, madeni yako hukatwa kwanza — . Mwanachama mpya hahudumiwi kabla ya kuthibitishwa — . Bereavement and celebration support follows , disaster support . Before any service, your debts are deducted first — . A new member is not served before confirmation — .
Kusitishwa kwa akaunti — Termination
Akaunti hufungwa pale uanachama unapokoma kwa sababu zozote za — ikiwemo kujiondoa kwa hiari, kutolipa ada miezi mitatu mfululizo, au kufukuzwa na mkutano wa wanaumoja kwa . An account closes when membership ends for any of the reasons in — including voluntary withdrawal, three consecutive months of unpaid dues, or expulsion by the members' meeting under .
Mipaka ya mfumo — Limits of the system
App ni chombo cha kumbukumbu — si mbadala wa vikao wala maamuzi ya umoja. Hitilafu ya kiufundi ikitokea, kumbukumbu husahihishwa na viongozi na masahihisho hubaki na alama ya aliyeyafanya. Chombo cha juu cha maamuzi kinabaki kuwa Mkutano Mkuu — . The app is a record-keeping tool — not a replacement for meetings or the group's decisions. If a technical fault occurs, records are corrected by the officers and corrections keep the mark of who made them. The supreme decision-making body remains the General Meeting — .
Mabadiliko ya masharti — Changes to these terms
Masharti haya husasishwa kila mfumo unapoongeza au kubadilisha kipengele, na toleo jipya hutangazwa kwenye Matangazo. Mabadiliko ya Katiba yenyewe ni ya Mkutano Mkuu pekee — ; Kanuni hubadilishwa na mkutano wa wanaumoja — . These terms are updated whenever the system adds or changes a feature, and each new version is announced in Notices. Changing the Constitution itself belongs only to the General Meeting — ; the Regulations are changed by the members' meeting — .
Viongozi Officers
Kutoa kadi ni kumkubali mwanachama. Andika kikao kilichoidhinisha —
kadi isiyo na rejea huonekana kama haijathibitishwa.
Issuing a code is the act of admitting a member. Name the meeting that
authorised it; a code without one is shown as unverified.
Deni ni madai yaliyotolewa bila malipo — halihifadhiwi popote, linahesabiwa. A debt is a charge raised and not yet paid; it is never stored, only worked out.
Kanuni 7 — madeni yanakatwa kwanza kabla ya kupewa huduma. Kanuni 7 — debts are deducted before any benefit is paid.
Unaona kuwa nyaraka ipo. Kuifungua kunahitaji ruhusa ya mwenye nyaraka.
You can see that a document exists. Opening it needs the owner's permission.
Mwanachama hapatikani na jambo ni la dharura? Unaweza kufungua — lakini kwa sababu iliyoandikwa, kwa siku 7, na atajulishwa mara moja. The member cannot be reached and the matter is urgent? You may open it — but with a reason on record, for 7 days, and they are told at once.
Kuhusu ukurasa huu About this page
Mambo yasiyoelezwa kwenye Katiba wala Kanuni. Mfumo hauamui kwa niaba ya umoja. Matters neither the Katiba nor the Kanuni settle. The system does not decide on the group's behalf.
- 1 Linaibuka Jambo halijaelezwa wazi kwenye Katiba wala Kanuni, hivyo swali huwekwa hapa badala ya kuachwa bila kumbukumbu.
- 2 Kanuni ya muda Kamati au mkutano huweka jinsi ya kuendelea kwa sasa, ili kazi isikwame ikisubiri uamuzi rasmi.
- 3 Uamuzi wa mwisho Chombo chenye mamlaka — mkutano mkuu au kamati iliyotajwa — hufanya uamuzi wa kudumu; swali huhamia kundi la "Yameamuliwa".
Kama Katibu: tumia orodha ya "Yanayosubiri uamuzi" kuandaa ajenda ya mkutano unaofuata.